Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?
Methali 28:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Heri mtu amchaye Mwenyezi-Mungu daima; lakini mkaidi wa moyo ataangukia maafa. Biblia Habari Njema - BHND Heri mtu amchaye Mwenyezi-Mungu daima; lakini mkaidi wa moyo ataangukia maafa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Heri mtu amchaye Mwenyezi-Mungu daima; lakini mkaidi wa moyo ataangukia maafa. Neno: Bibilia Takatifu Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Mwenyezi Mungu, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huanguka kwenye taabu. Neno: Maandiko Matakatifu Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha bwana, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huangukia kwenye taabu. BIBLIA KISWAHILI Mwanadamu mwenye kicho yu heri siku zote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara. |
Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?
Msifanye mioyo yenu kuwa migumu; Kama ilivyokuwa huko Meriba Kama siku ile katika Masa jangwani.
Na wale Wamisri wakawafuata, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi wote wa Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake.
Lakini waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na moyo wake Farao ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama BWANA alivyonena.
Ijapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia na akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake;
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha, ili niwatendee mema; nami nitatia kicho changu mioyoni mwao, ili wasiniache.
Vema. Yalikatwa kwa kutoamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.
Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,
Basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika pumziko lake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.
Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.