Je! Bwana wangu hakuambiwa nilivyofanya hapo Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA? Jinsi nilivyowaficha manabii wa BWANA, watu mia moja, hamsini hamsini katika pango, nikawalisha chakula na kuwapa maji?
Methali 28:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wema wakipata madaraka maisha hufana, lakini waovu wakitawala watu hujificha. Biblia Habari Njema - BHND Watu wema wakipata madaraka maisha hufana, lakini waovu wakitawala watu hujificha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wema wakipata madaraka maisha hufana, lakini waovu wakitawala watu hujificha. Neno: Bibilia Takatifu Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha. Neno: Maandiko Matakatifu Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha. BIBLIA KISWAHILI Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha. |
Je! Bwana wangu hakuambiwa nilivyofanya hapo Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA? Jinsi nilivyowaficha manabii wa BWANA, watu mia moja, hamsini hamsini katika pango, nikawalisha chakula na kuwapa maji?
Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote BWANA aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake.
Ndipo hao wakuu wakamwambia Baruku, Nenda ukajifiche, wewe na Yeremia, wala mtu asipajue mlipo.
Mfalme akamwamuru Yerameeli, mwana wa mfalme, na Seraya, mwana wa Azrieli, na Shelemia, mwana wa Abdeeli, wamkamate Baruku, mwandishi, na Yeremia, nabii; lakini BWANA aliwaficha.
Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.
Tena, baba yangu, tazama, tafadhali, tazama upindo wa vazi lako mkononi mwangu; maana ikiwa nimeukata upindo wa vazi lako, nisikuue, ujue, na kuona ya kuwa hakuna uovu wala kosa mkononi mwangu, wala sikukukosa neno; ingawa wewe unaniwinda roho yangu ili kuikamata.