Na yule mjumbe, aliyekwenda kumwita Mikaya, akamwambia, akasema, Angalia sasa, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja husema mema kwa mfalme; neno lako na liwe, nakusihi, kama neno la mmojawapo wao, ukaseme mema.
Methali 27:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amwamkiaye jirani kwa kelele alfajiri, itaeleweka kwamba amemtakia laana. Biblia Habari Njema - BHND Amwamkiaye jirani kwa kelele alfajiri, itaeleweka kwamba amemtakia laana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amwamkiaye jirani kwa kelele alfajiri, itaeleweka kwamba amemtakia laana. Neno: Bibilia Takatifu Mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kuwa ni laana. Neno: Maandiko Matakatifu Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kama ni laana. BIBLIA KISWAHILI Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake. |
Na yule mjumbe, aliyekwenda kumwita Mikaya, akamwambia, akasema, Angalia sasa, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja husema mema kwa mfalme; neno lako na liwe, nakusihi, kama neno la mmojawapo wao, ukaseme mema.
Ndipo mfalme wa Israeli akawakusanya pamoja manabii, kama watu mia nne. Akawaambia Je! Niende juu ya Ramoth-Gileadi kuupiga vita, au ninyamaze? Wakasema Kwea; kwa kuwa BWANA atautia mkononi mwa mfalme.
Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;