Hezekia akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele.
Methali 25:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Asiyetawala roho yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu asiyeweza kuzuia hasira yake, ni kama mji usio na ulinzi unaposhambuliwa. Biblia Habari Njema - BHND Mtu asiyeweza kuzuia hasira yake, ni kama mji usio na ulinzi unaposhambuliwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu asiyeweza kuzuia hasira yake, ni kama mji usio na ulinzi unaposhambuliwa. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile mji ambao kuta zake zimebomoka ndivyo alivyo mtu ambaye hawezi kujitawala mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile mji ambao kuta zake zimebomoka ndivyo alivyo mtu ambaye hawezi kujitawala mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Asiyetawala roho yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta. |
Hezekia akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele.
Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.
Basi hasira yake Sauli ikawaka juu ya Yonathani, akamwambia, Wewe, mwana wa mke mkaidi, asi, je! Mimi sijui ya kuwa umemchagua huyo mwana wa Yese, kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.
Basi sasa ujue na kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye.