Methali 25:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Upepo wa kusi huleta mvua, hali kadhalika masengenyo huleta chuki. Biblia Habari Njema - BHND Upepo wa kusi huleta mvua, hali kadhalika masengenyo huleta chuki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Upepo wa kusi huleta mvua, hali kadhalika masengenyo huleta chuki. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile upepo wa kaskazini uletavyo mvua, ndivyo ulimi usingiziao uletavyo uso wa hasira. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile upepo wa kaskazini uletavyo mvua, ndivyo ulimi usingiziao uletavyo uso wa hasira. BIBLIA KISWAHILI Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu. |
Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamwangamiza. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitamvumilia.
Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala kumtenda mwenziwe mabaya, Wala kumsengenya jirani yake.
wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong'onezo, na majivuno, na ghasia;