Labda BWANA atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye BWANA atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.
Methali 25:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo utafanya apate aibu kali, kama makaa ya moto kichwani pake, naye Mwenyezi-Mungu atakutuza. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo utafanya apate aibu kali, kama makaa ya moto kichwani pake, naye Mwenyezi-Mungu atakutuza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo utafanya apate aibu kali, kama makaa ya moto kichwani pake, naye Mwenyezi-Mungu atakutuza. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake, naye Mwenyezi Mungu atakupa thawabu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake, naye bwana atakupa thawabu. BIBLIA KISWAHILI Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu. |
Labda BWANA atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye BWANA atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.
Wakaondoka wale watu waliotajwa majina yao, wakawatwaa wafungwa, wakawavika kwa zile nyara wale wote waliokuwa uchi, wakawapa mavazi na viatu, wakawalisha, wakawanywesha, wakawatia mafuta, wakawapandisha waliokuwa dhaifu miongoni mwao juu ya punda wakawaleta Yeriko, mji wa mitende, kwa ndugu zao; kisha wakarudi Samaria.
Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Nawe umeonesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani BWANA aliponitia mikononi mwako, hukuniua.