Methali 25:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu atoaye ushahidi wa uongo dhidi ya mwenziwe, ni hatari kama rungu, upanga au mshale mkali. Biblia Habari Njema - BHND Mtu atoaye ushahidi wa uongo dhidi ya mwenziwe, ni hatari kama rungu, upanga au mshale mkali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu atoaye ushahidi wa uongo dhidi ya mwenziwe, ni hatari kama rungu, upanga au mshale mkali. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile rungu au upanga au mshale mkali ndivyo alivyo mtu atoaye ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile rungu au upanga au mshale mkali ndivyo alivyo mtu atoaye ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake. BIBLIA KISWAHILI Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali. |
Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na kukuchukia.
Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA.
Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea.
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.