Methali 25:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa uvumilivu mtawala huweza kushawishika; ulimi laini huvunja mifupa. Biblia Habari Njema - BHND Kwa uvumilivu mtawala huweza kushawishika; ulimi laini huvunja mifupa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa uvumilivu mtawala huweza kushawishika; ulimi laini huvunja mifupa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini unaweza kuvunja mfupa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa. BIBLIA KISWAHILI Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa. |
Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.
Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.
Akatwaa asali mikononi mwake akasonga mbele, huku akila alipokuwa akienda, akawafikia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.
Lakini kijana mmojawapo alimpasha habari Abigaili, mkewe Nabali, akasema, Tazama, Daudi alituma wajumbe kutoka nyikani waje ili kumsalimu bwana wetu, naye akawatukana.