Wakamzika Abneri katika Hebroni; naye mfalme akapaza sauti yake, akalia kaburini kwa Abneri, nao watu wote wakalia.
Methali 24:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake, Biblia Habari Njema - BHND Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake, Neno: Bibilia Takatifu Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati anapojikwaa, usiruhusu moyo wako ushangilie. Neno: Maandiko Matakatifu Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie. BIBLIA KISWAHILI Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; |
Wakamzika Abneri katika Hebroni; naye mfalme akapaza sauti yake, akalia kaburini kwa Abneri, nao watu wote wakalia.
Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu;
Lakini nikijikwaa wanafurahi na kukusanyana, Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua, Wakanipapura bila kukoma.
Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao.
Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu.
Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.