Methali 24:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, ule asali maana ni nzuri; sega la asali ni tamu mdomoni. Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, ule asali maana ni nzuri; sega la asali ni tamu mdomoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, ule asali maana ni nzuri; sega la asali ni tamu mdomoni. Neno: Bibilia Takatifu Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka sega ni tamu kwa kuonja. Neno: Maandiko Matakatifu Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja. BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. |
Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.
Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.
Bibi arusi, midomo yako yadondosha asali, Asali na maziwa viko chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.
Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bibi arusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.
Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Akatwaa asali mikononi mwake akasonga mbele, huku akila alipokuwa akienda, akawafikia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.
Ila Yonathani hakusikia, hapo babaye alipowaagiza watu kwa kiapo; basi yeye akainyosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake, na kuichovya katika sega la asali, kisha akatia mkono wake kinywani; na macho yake yakatiwa nuru.