Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, kisha mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, na wenye ujasiri.
Methali 23:34 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utakuwa kama mtu alalaye katikati ya bahari, kama mtu alalaye juu ya mlingoti wa meli. Biblia Habari Njema - BHND Utakuwa kama mtu alalaye katikati ya bahari, kama mtu alalaye juu ya mlingoti wa meli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utakuwa kama mtu alalaye katikati ya bahari, kama mtu alalaye juu ya mlingoti wa meli. Neno: Bibilia Takatifu Utakuwa kama alalaye baharini, alalaye juu ya kamba ya merikebu. Neno: Maandiko Matakatifu Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari, alalaye juu ya kamba ya merikebu. BIBLIA KISWAHILI Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. |
Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, kisha mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, na wenye ujasiri.
Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamlia njama; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza;
Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa kilima, Vilindi vikagandamana katikati ya bahari.
Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Kiko wapi kileo?
Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hadi siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;