Methali 23:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, nisikilize kwa makini, shikilia mwenendo wa maisha yangu. Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, nisikilize kwa makini, shikilia mwenendo wa maisha yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, nisikilize kwa makini, shikilia mwenendo wa maisha yangu. Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, nipe moyo wako, macho yako na yafuate njia zangu, Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, nipe moyo wako, macho yako na yafuate njia zangu, BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. |
Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wa kiume na wa kike; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.
Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa iangazayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.