Methali 23:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nunua ukweli, wala usiuuze; nunua hekima, mafunzo na busara. Biblia Habari Njema - BHND Nunua ukweli, wala usiuuze; nunua hekima, mafunzo na busara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nunua ukweli, wala usiuuze; nunua hekima, mafunzo na busara. Neno: Bibilia Takatifu Nunua kweli wala usiiuze, pata hekima, adabu na ufahamu. Neno: Maandiko Matakatifu Nunua kweli wala usiiuze, pata hekima, adabu na ufahamu. BIBLIA KISWAHILI Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu. |
Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila gharama.
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja.
akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.