Methali 23:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwanangu, kama moyo wako una hekima, Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, moyo wako ukiwa wenye busara, moyo wangu pia utakuwa wenye furaha. Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, moyo wako ukiwa wenye busara, moyo wangu pia utakuwa wenye furaha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, moyo wako ukiwa wenye busara, moyo wangu pia utakuwa wenye furaha. Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, kama moyo wako una hekima, basi moyo wangu utafurahi, Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, kama moyo wako una hekima, basi moyo wangu utafurahi, BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, kama moyo wako una hekima, Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu; |
Naam, nitafurahi juu yao niwatendee mema, nami nitawapanda katika nchi hii kweli kweli, kwa moyo wangu wote, na kwa roho yangu yote.
BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.
Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, akiwa amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Bali ilibidi kusherehekea na kushangilia kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.
Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
Nilifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.