Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.
Methali 23:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana Mungu, Mkombozi, ni mwenye nguvu, naye ataitetea haki yao dhidi yako. Biblia Habari Njema - BHND maana Mungu, Mkombozi, ni mwenye nguvu, naye ataitetea haki yao dhidi yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana Mungu, Mkombozi, ni mwenye nguvu, naye ataitetea haki yao dhidi yako. Neno: Bibilia Takatifu kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu, atawatetea dhidi yako. Neno: Maandiko Matakatifu kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu, atalichukua shauri lao dhidi yako. BIBLIA KISWAHILI Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako. |
Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Mungu huwapa wapweke makao yao; Huwapa wafungwa uhuru na kuwafanikisha; Bali wakaidi huishi katika nchi kavu.
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu.
Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.