ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.
Methali 21:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini BWANA ndiye aletaye wokovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Farasi hutayarishwa kwa vita, lakini ushindi wamtegemea Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Farasi hutayarishwa kwa vita, lakini ushindi wamtegemea Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Farasi hutayarishwa kwa vita, lakini ushindi wamtegemea Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa bwana. BIBLIA KISWAHILI Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini BWANA ndiye aletaye wokovu. |
ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA!
Ni kweli, msaada haufai unaotazamiwa kutoka milimani, makutano yenye mshindo juu ya milima; ni kweli, wokovu wa Israeli ni katika BWANA, Mungu wetu.