Methali 21:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sadaka ya wasio haki ni chukizo; Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tambiko ya mwovu ni kitu cha kuchukiza, huchukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya. Biblia Habari Njema - BHND Tambiko ya mwovu ni kitu cha kuchukiza, huchukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tambiko ya mwovu ni kitu cha kuchukiza, huchukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya. Neno: Bibilia Takatifu Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo; si ni chukizo zaidi ikitolewa kwa nia mbaya! Neno: Maandiko Matakatifu Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo, si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya! BIBLIA KISWAHILI Sadaka ya wasio haki ni chukizo; Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya! |
Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.
Yeye achinjaye ng'ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.
Yafaa nini niletewe ubani kutoka Sheba, na udi kutoka nchi iliyo mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliwi, wala dhabihu zenu haziniridhii.
Musa akakasirika sana, akamwambia BWANA. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao.
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.