Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu.
Methali 21:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri; tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu. Biblia Habari Njema - BHND Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri; tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri; tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu. Neno: Bibilia Takatifu Zawadi inayotolewa kwa siri hutuliza hasira, na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. Neno: Maandiko Matakatifu Zawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. BIBLIA KISWAHILI Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni hutuliza ghadhabu kali. |
Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu.
Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.
Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa.
Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimelikubali ombi lako.