Methali 20:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wema na uaminifu humkinga mfalme; utawala wake huimarishwa kwa uadilifu. Biblia Habari Njema - BHND Wema na uaminifu humkinga mfalme; utawala wake huimarishwa kwa uadilifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wema na uaminifu humkinga mfalme; utawala wake huimarishwa kwa uadilifu. Neno: Bibilia Takatifu Upendo na uaminifu humweka mfalme salama; kiti chake cha ufalme huwa salama kwa upendo. Neno: Maandiko Matakatifu Upendo na uaminifu humweka mfalme salama, kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama. BIBLIA KISWAHILI Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili. |
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.
tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye Juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme;