BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Methali 20:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Dhamiri ya mtu ni taa ya Mwenyezi-Mungu; huchunguza nafsi yake mtu mpaka ndani kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Dhamiri ya mtu ni taa ya Mwenyezi-Mungu; huchunguza nafsi yake mtu mpaka ndani kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Dhamiri ya mtu ni taa ya Mwenyezi-Mungu; huchunguza nafsi yake mtu mpaka ndani kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Taa ya Mwenyezi Mungu huchunguza roho ya mwanadamu, huchunguza utu wake wa ndani. Neno: Maandiko Matakatifu Taa ya bwana huchunguza roho ya mwanadamu, huchunguza utu wake wa ndani. BIBLIA KISWAHILI Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake. |
BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili.
Hao waionesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;
Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.