Methali 20:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayemlaani baba yake au mama yake, mwanga wa uhai wake utazimwa kama taa gizani. Biblia Habari Njema - BHND Anayemlaani baba yake au mama yake, mwanga wa uhai wake utazimwa kama taa gizani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayemlaani baba yake au mama yake, mwanga wa uhai wake utazimwa kama taa gizani. Neno: Bibilia Takatifu Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itazimwa katika giza nene. Neno: Maandiko Matakatifu Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itazimwa katika giza nene. BIBLIA KISWAHILI Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu. |
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.
Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa, amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake.
Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.
Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.