Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
Methali 20:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usipende kulala tu usije ukawa maskini; uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi. Biblia Habari Njema - BHND Usipende kulala tu usije ukawa maskini; uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usipende kulala tu usije ukawa maskini; uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi. Neno: Bibilia Takatifu Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba. Neno: Maandiko Matakatifu Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba. BIBLIA KISWAHILI Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. |
Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.
Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.
Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu uko karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.
Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.