Nami ninajua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao.
Methali 19:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Haja ya mwanadamu ni hisani yake; Ni afadhali maskini kuliko mwongo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kinachotakiwa kwa mtu ni uaminifu; afadhali mtu maskini kuliko mtu mwongo. Biblia Habari Njema - BHND Kinachotakiwa kwa mtu ni uaminifu; afadhali mtu maskini kuliko mtu mwongo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kinachotakiwa kwa mtu ni uaminifu; afadhali mtu maskini kuliko mtu mwongo. Neno: Bibilia Takatifu Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho, afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo. Neno: Maandiko Matakatifu Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho, afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo. BIBLIA KISWAHILI Haja ya mwanadamu ni hisani yake; Ni afadhali maskini kuliko mwongo. |
Nami ninajua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao.
Lakini BWANA akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako;
Ndugu zangu wametenda udanganyifu kama kijito cha maji. Mfano wa fumbi la vijito vipitavyo.
Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.
katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele;