Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu watu hawa wako walio wengi?
Methali 18:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mwenye akili hujipatia maarifa, sikio la mwenye busara hutafuta maarifa. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mwenye akili hujipatia maarifa, sikio la mwenye busara hutafuta maarifa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mwenye akili hujipatia maarifa, sikio la mwenye busara hutafuta maarifa. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa. BIBLIA KISWAHILI Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa. |
Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu watu hawa wako walio wengi?
mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
Naye alikuwa na dada yake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.