Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu;
Methali 17:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amchekaye maskini humtukana Muumba wake; Naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayemdhihaki maskini anamtukana Muumba wake; anayefurahia maafa hatakosa kuadhibiwa. Biblia Habari Njema - BHND Anayemdhihaki maskini anamtukana Muumba wake; anayefurahia maafa hatakosa kuadhibiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayemdhihaki maskini anamtukana Muumba wake; anayefurahia maafa hatakosa kuadhibiwa. Neno: Bibilia Takatifu Yeye anaye mdhihaki maskini huonesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa. BIBLIA KISWAHILI Amchekaye maskini humtukana Muumba wake; Naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu. |
Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu;
Mimi hapa sikufanya haraka kuacha kuwa mchungaji nyuma yako; wala sikuitamani siku ya maradhi ya kuua; wewe unajua; yaliyotoka midomoni mwangu yalikuwa mbele za uso wako.
Uwaambie hao wana wa Amoni, Lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umesema, Aha! Juu ya patakatifu pangu, palipotiwa unajisi; na juu ya nchi ya Israeli, ilipoharibiwa; na juu ya nyumba ya Israeli, walipokwenda kifungoni;
Kwa sababu ya udhalimu aliotendwa ndugu yako Yakobo, aibu itakufunika, nawe utakatiliwa mbali hata milele.
Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kuyumbayumba, nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe.
Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?