Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako.
Methali 17:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenye kulipiza mema kwa mabaya, mabaya hayataondoka nyumbani mwake. Biblia Habari Njema - BHND Mwenye kulipiza mema kwa mabaya, mabaya hayataondoka nyumbani mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenye kulipiza mema kwa mabaya, mabaya hayataondoka nyumbani mwake. Neno: Bibilia Takatifu Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake. Neno: Maandiko Matakatifu Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake. BIBLIA KISWAHILI Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake. |
Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako.
Kisha nitaifanya nyumba yako iwe kama nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa ajili ya chukizo ulilonichukiza, hata kunighadhibisha, ukawakosesha Israeli.
Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.
Naye Yonathani akamsifu Daudi kwa Sauli, babaye akamwambia, Mfalme asikose juu ya mtumishi wake, yaani, juu ya Daudi kwa maana yeye hakukosa juu yako, tena matendo yake kwako yamekuwa mema sana.
Akamwambia Daudi, Wewe u mwenye haki kuliko mimi; maana wewe umenitendea mema, nami nimekutenda mabaya.
Basi Daudi alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo mtu huyu, asipotewe na kitu chochote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya badala ya mema.