Methali 16:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu mshupavu huleta fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mpotovu hueneza ugomvi, mfitini hutenganisha marafiki. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mpotovu hueneza ugomvi, mfitini hutenganisha marafiki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mpotovu hueneza ugomvi, mfitini hutenganisha marafiki. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi huwatenganisha rafiki wa karibu. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu. BIBLIA KISWAHILI Mtu mshupavu huleta fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki. |
Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.
Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong'onezo, na majivuno, na ghasia;
Daudi akamwambia Sauli, Kwa nini unasikiliza maneno ya watu wasemao, Tazama, Daudi anataka kukudhuru?