Methali 16:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maneno mazuri ni kama asali; ni matamu rohoni na yenye kuupa mwili afya. Biblia Habari Njema - BHND Maneno mazuri ni kama asali; ni matamu rohoni na yenye kuupa mwili afya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maneno mazuri ni kama asali; ni matamu rohoni na yenye kuupa mwili afya. Neno: Bibilia Takatifu Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa. Neno: Maandiko Matakatifu Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa. BIBLIA KISWAHILI Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani. |
Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.
Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.
Huyo Mhubiri akachunguza ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli.
Bibi arusi, midomo yako yadondosha asali, Asali na maziwa viko chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.
Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA, Mungu wa majeshi.
Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.
Nikakitwaa kile kitabu kidogo kutoka mkononi mwa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu.