Je! Yapasa mtu mwenye hekima kujibu kwa ujuzi wa uvuvio, Na kulijaza tumbo lake upepo wa mashariki?
Methali 16:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Moyo wa mwenye hekima humwezesha kusema kwa busara; huyafanya maneno yake yawe ya kuvutia. Biblia Habari Njema - BHND Moyo wa mwenye hekima humwezesha kusema kwa busara; huyafanya maneno yake yawe ya kuvutia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Moyo wa mwenye hekima humwezesha kusema kwa busara; huyafanya maneno yake yawe ya kuvutia. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho. BIBLIA KISWAHILI Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake. |
Je! Yapasa mtu mwenye hekima kujibu kwa ujuzi wa uvuvio, Na kulijaza tumbo lake upepo wa mashariki?
Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.
Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.