Methali 15:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mdomo wa mwenye hekima hueneza maarifa, lakini sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. Biblia Habari Njema - BHND Mdomo wa mwenye hekima hueneza maarifa, lakini sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mdomo wa mwenye hekima hueneza maarifa, lakini sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. Neno: Bibilia Takatifu Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. Neno: Maandiko Matakatifu Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. BIBLIA KISWAHILI Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo. |
Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.
Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kulia; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.
Bibi arusi, midomo yako yadondosha asali, Asali na maziwa viko chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.
Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba.
Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha wengine vile vile.
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.