Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.
Methali 15:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sikio lisikilizalo lawama yenye uhai Litakaa kati yao wenye hekima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu ambaye husikiliza maonyo mema, anayo nafasi yake miongoni mwa wenye hekima. Biblia Habari Njema - BHND Mtu ambaye husikiliza maonyo mema, anayo nafasi yake miongoni mwa wenye hekima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu ambaye husikiliza maonyo mema, anayo nafasi yake miongoni mwa wenye hekima. Neno: Bibilia Takatifu Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima atakuwa miongoni mwa wenye hekima. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima atakuwa miongoni mwa wenye hekima. BIBLIA KISWAHILI Sikio lisikilizalo lawama yenye uhai Litakaa kati yao wenye hekima. |
Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.
Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa.
Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.
Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.