Methali 15:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Moyo wa mwadilifu hufikiri kabla ya kujibu, lakini kinywa cha mwovu hububujika uovu. Biblia Habari Njema - BHND Moyo wa mwadilifu hufikiri kabla ya kujibu, lakini kinywa cha mwovu hububujika uovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Moyo wa mwadilifu hufikiri kabla ya kujibu, lakini kinywa cha mwovu hububujika uovu. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya. BIBLIA KISWAHILI Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya. |
Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa; Bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.
Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.
Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba hukukusudia; kwa nini Mungu akasirishwe na maneno yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?
Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa heshima.
Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;