Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.
Methali 15:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ushauri mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maneno yapendezayo ni safi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mawazo ya mwovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, bali maneno mema humfurahisha. Biblia Habari Njema - BHND Mawazo ya mwovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, bali maneno mema humfurahisha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mawazo ya mwovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, bali maneno mema humfurahisha. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye. Neno: Maandiko Matakatifu bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye. BIBLIA KISWAHILI Ushauri mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maneno yapendezayo ni safi. |
Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.
Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?
Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;