Methali 15:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Chakula cha mboga palipo na upendo; Ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na kuchukiana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Afadhali mlo wa jioni wa mchicha na upendo, kuliko karamu ya nyama nono pamoja na chuki. Biblia Habari Njema - BHND Afadhali mlo wa jioni wa mchicha na upendo, kuliko karamu ya nyama nono pamoja na chuki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Afadhali mlo wa jioni wa mchicha na upendo, kuliko karamu ya nyama nono pamoja na chuki. Neno: Bibilia Takatifu Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo, kuliko nyama ya ndama aliyenona pamoja na chuki. Neno: Maandiko Matakatifu Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki. BIBLIA KISWAHILI Chakula cha mboga palipo na upendo; Ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na kuchukiana. |
Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo.
Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.
Basi ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyote na rehema,
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.