Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitashuka kaburini kwa mwanangu, nikiomboleza. Basi baba yake akamlilia.
Methali 15:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Siku zote za mtu ateswaye ni mbaya; Bali ukunjufu wa moyo ni karamu ya daima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa mnyonge kila siku ni mbaya, lakini kwa mwenye moyo mchangamfu ni sikukuu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa mnyonge kila siku ni mbaya, lakini kwa mwenye moyo mchangamfu ni sikukuu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa mnyonge kila siku ni mbaya, lakini kwa mwenye moyo mchangamfu ni sikukuu. Neno: Bibilia Takatifu Siku zote za wanaoteswa ni za taabu, bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu. Neno: Maandiko Matakatifu Siku zote za wanaoonewa ni za taabu, bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu. BIBLIA KISWAHILI Siku zote za mtu ateswaye ni mbaya; Bali ukunjufu wa moyo ni karamu ya daima. |
Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitashuka kaburini kwa mwanangu, nikiomboleza. Basi baba yake akamlilia.
Yakobo akamjibu Farao, Siku za kuishi kwangu ni miaka mia moja na thelathini; siku za maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikia siku za maisha ya baba zangu katika siku za kuishi kwao.
Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
Lakini ilipokuwa karibu usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.
Kwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu; si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu; tulienenda katika dunia, na hasa kwenu ninyi.
Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili pia katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.