Farao akawaambia watumishi wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye Roho ya Mungu ndani yake?
Methali 14:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme humfadhili mtumishi atendaye kwa hekima, lakini hasira yake huwakumba watendao yasiyofaa. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme humfadhili mtumishi atendaye kwa hekima, lakini hasira yake huwakumba watendao yasiyofaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme humfadhili mtumishi atendaye kwa hekima, lakini hasira yake huwakumba watendao yasiyofaa. Neno: Bibilia Takatifu Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima, bali ghadhabu yake humwangukia mtumishi mwenye kuaibisha. Neno: Maandiko Matakatifu Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima, bali ghadhabu yake humwangukia mtumishi mwenye kuaibisha. BIBLIA KISWAHILI Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu. |
Farao akawaambia watumishi wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye Roho ya Mungu ndani yake?
Mfalme akaondoka kwa ghadhabu kutoka kwenye karamu ya divai, akaingia bustani ya ngome. Hamani naye akasimama ili ajitakie maisha yake kwa malkia Esta; kwa kuwa aliona ya kwamba amekusudiwa madhara na mfalme.
Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.
Mfalme mwenye hekima huwapepeta wasio haki; Naye hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.