Methali 14:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayemdhulumu maskini anamtukana Muumba wake, lakini amwoneaye huruma mhitaji anamtukuza Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Anayemdhulumu maskini anamtukana Muumba wake, lakini amwoneaye huruma mhitaji anamtukuza Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayemdhulumu maskini anamtukana Muumba wake, lakini amwoneaye huruma mhitaji anamtukuza Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Yeye anayemdhulumu maskini humdharau Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu. BIBLIA KISWAHILI Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. |
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri.
Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako;