Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Methali 14:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Fahari ya mfalme ni wingi wa watu wake, lakini bila watu mtawala huangamia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Fahari ya mfalme ni wingi wa watu wake, lakini bila watu mtawala huangamia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Fahari ya mfalme ni wingi wa watu wake, lakini bila watu mtawala huangamia.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme, bali pasipo watu mkuu huangamia.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme, bali pasipo watu mkuu huangamia.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Methali 14:28
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi sasa, ondoka, utoke nje, ukaseme na watumishi wako maneno ya kuwatuliza roho zao; maana mimi nakuapia kwa BWANA, usipotoka, hatabaki hata mtu mmoja pamoja nawe usiku huu; na mambo haya yatakuwa mabaya kwako kuliko mabaya yote yaliyokupata tokea ujana wako hadi sasa.


Naye Yoabu akamwambia mfalme, BWANA, Mungu wako, na awaongeze watu, hesabu yao ikiwa yoyote, mara mia, tena macho ya bwana wangu mfalme na yawaone; ila kwa nini neno hili limempendeza bwana wangu mfalme?


Wana wa Israeli nao wakahesabiwa, wakapewa vyakula, wakaenda kupigana nao; wakatua wana wa Israeli mbele yao kama vikundi viwili vya wana-mbuzi; bali Washami wakaijaza nchi.


Kwa kuwa hakumwachia Yehoahazi watu ila wapandao farasi hamsini, na magari kumi, na askari elfu kumi waendao kwa miguu; kwa kuwa mfalme wa Shamu aliwaharibu, akawaponda mfano wa mavumbi yaliyokanyagwa.


Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Ndipo Wamisri wakaogopa kwa sababu ya wana wa Israeli.


Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake wote, akisema, Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto wa kike mtamhifadhi hai.


Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.


Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.


Inua macho yako, Ee Yerusalemu, ukawatazame hawa wanaokuja kutoka kaskazini; liko wapi kundi lako ulilopewa, kundi lile zuri?