Methali 14:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayemdharau jirani yake ni mwenye dhambi, bali ana heri aliye mwema kwa maskini. Biblia Habari Njema - BHND Anayemdharau jirani yake ni mwenye dhambi, bali ana heri aliye mwema kwa maskini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayemdharau jirani yake ni mwenye dhambi, bali ana heri aliye mwema kwa maskini. Neno: Bibilia Takatifu Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji. BIBLIA KISWAHILI Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri. |
Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
Maana hapuuzi Wala kuchukizwa na mateso ya anayeteswa, Wala hamfichi uso wake, Bali humsikia akimlilia.
Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.
Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka.
Akawaambia mfano huu watu waliojiamini ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.