Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?
Methali 14:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mjinga huamini kila kitu anachoambiwa, lakini mwenye busara huwa na tahadhari. Biblia Habari Njema - BHND Mjinga huamini kila kitu anachoambiwa, lakini mwenye busara huwa na tahadhari. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mjinga huamini kila kitu anachoambiwa, lakini mwenye busara huwa na tahadhari. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mjinga huamini kila kitu, bali mwenye busara hufikiria hatua zake. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mjinga huamini kila kitu, bali mwenye busara hufikiria hatua zake. BIBLIA KISWAHILI Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. |
Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?
Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu; Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.
Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.
mtu huyu alikuwa pamoja na mtawala Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye mtawala akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.