Methali 14:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi. Biblia Habari Njema - BHND Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi. Neno: Bibilia Takatifu Hata katika kicheko moyo unaweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi. Neno: Maandiko Matakatifu Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi. BIBLIA KISWAHILI Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo. |
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha basi ujifurahishe kwa anasa. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili.
Abrahamu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo yako mema katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unateseka.
Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni kubwa.