Methali 12:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mawazo ya mwadilifu ni ya haki; mashauri ya mwovu ni ya udanganyifu. Biblia Habari Njema - BHND Mawazo ya mwadilifu ni ya haki; mashauri ya mwovu ni ya udanganyifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mawazo ya mwadilifu ni ya haki; mashauri ya mwovu ni ya udanganyifu. Neno: Bibilia Takatifu Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki, bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu. Neno: Maandiko Matakatifu Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki, bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu. BIBLIA KISWAHILI Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa. |
Haja ya mwenye haki ni kupata mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu huishia katika ghadhabu.
Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?
Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA.
Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoesha ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu.
Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi.
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.