Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Methali 12:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Maneno ya ovyo hujeruhi kama upanga, lakini asemayo mwenye hekima huponesha kidonda.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Maneno ya ovyo hujeruhi kama upanga, lakini asemayo mwenye hekima huponesha kidonda.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Maneno ya ovyo hujeruhi kama upanga, lakini asemayo mwenye hekima huponesha kidonda.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Methali 12:18
17 Marejeleo ya Msalaba  

Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila.


Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.


Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.


Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye?


Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale,


Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila.


Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya.


Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.


Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.


Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.


Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali.


Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.


Na hao wenye hekima katika watu watafundisha wengi; hata hivyo wataanguka kwa upanga, na kwa moto, na kwa kufungwa, na kwa kutekwa nyara, siku nyingi.


Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kulia; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.


katikati ya njia yake kuu. Na upande huu na huu kando ya ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.