Methali 11:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mkarimu hufaidika yeye mwenyewe, lakini mtu mkatili hujiumiza mwenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mkarimu hufaidika yeye mwenyewe, lakini mtu mkatili hujiumiza mwenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mkarimu hufaidika yeye mwenyewe, lakini mtu mkatili hujiumiza mwenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe, bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe, bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake. |
Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Mwenye haki hupotea, wala hakuna atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya.
Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka.
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.