Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Methali 10:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa; Bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika, lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika, lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika, lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Midomo ya wenye haki hujua kile chenye kibali, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa; Bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Methali 10:32
13 Marejeleo ya Msalaba  

Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.


Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.


Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.


Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.


Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.


Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka;


Jiepushe na kinywa cha ujeuri, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.


Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotovu.


Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.


Huyo Mhubiri akachunguza ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli.


Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka.


na maneno yafaayo yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.