Methali 1:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema basi, mtakula matunda ya mienendo yenu, mtavimbiwa kwa hila zenu wenyewe. Biblia Habari Njema - BHND basi, mtakula matunda ya mienendo yenu, mtavimbiwa kwa hila zenu wenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza basi, mtakula matunda ya mienendo yenu, mtavimbiwa kwa hila zenu wenyewe. Neno: Bibilia Takatifu watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao. Neno: Maandiko Matakatifu watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. |
Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua nisiyoyafurahia.
Na watu hao, waliopewa unabii na wao, watatupwa nje katika njia kuu za Yerusalemu kwa sababu ya upanga na njaa; wala hawatakuwa na mtu wa kuwazika, wao na wake zao, na wana wao, na binti zao; maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.
Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Nami nitawaadhibu kwa kadiri ya matendo yenu, asema BWANA; nami nitawasha moto katika msitu wake, nao utateketeza vitu vyote viuzungukavyo.
Sikia, Ee nchi; tazama, nitaleta mabaya juu ya watu hawa, naam, matunda ya mawazo yao, kwa sababu hawakuyasikiliza maneno yangu; tena kwa habari ya sheria yangu, wameikataa.
Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.