Methali 1:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua; njoo tukawashambulie wasio na hatia! Biblia Habari Njema - BHND Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua; njoo tukawashambulie wasio na hatia! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua; njoo tukawashambulie wasio na hatia! Neno: Bibilia Takatifu Wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia; Neno: Maandiko Matakatifu Kama wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia; BIBLIA KISWAHILI Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; |
Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
Lakini mimi nilikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.
Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huvizia kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.
Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.
Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tuko tayari kumwua kabla hajakaribia.
na kumwomba fadhili juu yake, kwamba atoe amri aletwe Yerusalemu, wapate kumwotea na kumwua njiani.