Mathayo 27:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hadi saa tisa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, giza likaikumba nchi yote. Biblia Habari Njema - BHND Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, giza likaikumba nchi yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, giza likaikumba nchi yote. Neno: Bibilia Takatifu Tangu saa sita hadi saa tisa giza liliifunika nchi yote. Neno: Maandiko Matakatifu Tangu saa sita hadi saa tisa giza liliifunika nchi yote. BIBLIA KISWAHILI Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hadi saa tisa. |
Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana.
Nayo ilikuwa Maandalio ya Pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!
Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, na usiku vivyo hivyo.
Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuri kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.