Ndipo akakaribia Sedekia, mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Roho ya BWANA alitokaje kwangu ili aseme na wewe?
Mathayo 26:67 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo wakamtemea mate usoni, wakampiga ngumi; na wengine wakampiga makofi, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makofi. Wengine wakiwa wanampiga makofi, Biblia Habari Njema - BHND Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makofi. Wengine wakiwa wanampiga makofi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makofi. Wengine wakiwa wanampiga makofi, Neno: Bibilia Takatifu Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi Neno: Maandiko Matakatifu Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi BIBLIA KISWAHILI Ndipo wakamtemea mate usoni, wakampiga ngumi; na wengine wakampiga makofi, |
Ndipo akakaribia Sedekia, mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Roho ya BWANA alitokaje kwangu ili aseme na wewe?
Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.
Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Ndipo Pashuri akampiga Yeremia, nabii, akamtia katika mkatale, uliokuwa pale penye lango la juu la Benyamini, lililokuwa katika nyumba ya BWANA.
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
BWANA akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.
Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.
nao watamdhihaki, na kumtemea mate, na kumpiga mijeledi, na kumwua; na baada ya siku tatu atafufuka.
Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakamchukua wakampiga makofi.
Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani Mkuu?
tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kama takataka za dunia, na kuwa duni ya vitu vyote hata sasa.
ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.