Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.
Mathayo 25:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao. Biblia Habari Njema - BHND Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao. Neno: Bibilia Takatifu lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. Neno: Maandiko Matakatifu lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. BIBLIA KISWAHILI bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. |
Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.